Posts

Showing posts from February, 2020

KILIMO BORA CHA NYANYA

Image
KILIMO BORA CHA NYANYA 1.0 UTANGULIZI Nchini Tanzania zao la nyanya hulimwa karibu katika mikoa yote hasa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Tanga, Pwani na Mbeya. Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia kanuni bora za kilimo pamoja na udhibiti wa magonjwa na wadudu wa zao hili. Kwa manispaa ya Musoma zao la nyanya hulimwa na wakulima hulitegemea zao hili kama zao la biashara kwa kuwa huwapatia faida kubwa ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga. Halmashauri ya Manispaa ya Musoma imelipa kipaumbele zao hili kwa kulichagu zao hili na kuliweka kwenye mnyororo wa thamani kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora cha zao la nyan...

KILIMO CHA VITUNGUU

Image
UTANGULIZI Vitunguu maji kwa kitaalamu hujulikana kama Allium cepa na kwa kiingereza huitwa Bulb Onions. Vitunguu ni zao muhimu sana sio kwa matumizi ya ndani tu lakini pia ni zao la kibiashara linaloweza kukuletea kipato kikubwa.   Vitunguu ni zao la bustani  (Horticultural crop) ambalo lipo kwenye kundi la mboga mboga (vegetables). Zao hili ni maarufu kutokana na thamani ya virutubisho ilivyonavyo na ladha yake kwenye mapishi ya vyakula mbalimbali. Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo wa familia za kitanzania. Afrika Mashariki, na Dunia Nzima. MATUMIZI YA VITUNGUU Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia hutumika kutengeneza supu n.k KILIMO Nchini mwetu vitunguu hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tanga,  Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogor...