UFUNGAJI WA KUKU WA BROILER
Kijan amk huu mwaka uwe wa mafanikio kwako fanya vitu kwa malengo na kwa manufaa ya baadaye simple tuuuuuuuh wazo moja jingine mfano ukaamua kufuga kuku wanyam yani kwajin halis (BROILER) kuku haw wanafaid ya harak San maan kuku hawa wanakuwa kwa wiki 4 tuuuuuuuh unaweza kuwauza ss ukaamua kufug kuku wa nyama Mia 2 wananakul si zaid ya mifuko ya chakula 15 wakiwa vifarang ndani ya wiki 1 na nusu wanakula mfuko 1 na nusu baada ya hap wanaanza kula chakula grower ndani ya wiki moja na nusu kwahy wanakuw wamefikish wiki 3 wanakula mifuko 5 ya Growther ss wiki ya nne wanakula chakula mifuko 5 ya finisher hao nikuku Mia 2 tu ambao kuku 1 ni shilingi 6500 kwhy kuku 200 watakupa shlng million 1 na laki 3 kwahy bei ya chakula na matumiz mengine itakuw si zaid ya shilng laki 8 kwahy faida yako itakuw ni shlng laki 5 unakuwa huna hasar. Ss tunakuj kwa kuku Mia 500 hawa kuku wanamaliza mifuko ya chakula isiyozid 22 pak kufikia hatua ya kuchinja hizo wiki 4 kwahy mifuko ya starter watakul 3 growther mifuko 7 na finisher watakul mifuko 8 na hao kuku 1 ni shlng 6500 kwahy kuku 500 watakupa shlng 3250000 ukitow hel ya chakula na dawa ni shlng 2250000 kwahy ww utakuwa umebaki na faida ya shlng million 1 tuuuuuuuh kwahy kwaushaur wang ukifany ufugaji wa kisasa utanufaik zaid na zaid. Usikae kimya jiongeze kijan muda wakupang malengo yako ndo huuu. NEVER GIVE UP
UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)
Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.
Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba
· Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.
· Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.
· Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.
kutosha na kuepuka stress.
· Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.
Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba
· Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.
· Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.
· Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.
· Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.
Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35
MAJI
· Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida)
· Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.
CHAKULA
· Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders. Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).
· Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.
· Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.
U welcome to start
ReplyDelete